fcntv

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
  • HOME
  • RATIBA ZA VIPINDI
  • UDHAMINI
    • PIGA SIMU
    • EMAIL
    • SMS
  • MALIPO YA HUDUMA
  • MATANGAZO
  • MATAWI YETU
    • Dodoma
    • Igunga
    • Kahama
  • HABARI
  • MAGAZETI
  • VIDEO MPYA

skip to main | skip to sidebar
Home » HABARI » RAIS MAGUFULI AWAGEUKIA MUHIMBILI

RAIS MAGUFULI AWAGEUKIA MUHIMBILI



Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili sambamba na kumsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Hussein Kidantu na kumteua Prof. Lawrence Mseru kushika nafasi hiyo.
Kati ya maagizo Rais aliyoacha ni pamoja na mashine za CT Scan pamoja na MRIkuhakikisha zinatengenezwa ndani ya wiki mbili.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaisha amesema baada ya kukutana na kamati tendaji ya hospitali hiyo leo na Kaimu Mkurugenzi aliyeteuliwa Prof.Lawrence Mseru ametoa maelezo na kuhakikisha watafanyia kazi maagizo 
Yaliyotolewa na Rais ndani ya muda waliopewa.
“Tayari suala la CT Scan na MRI limeanza kufanyiwa kazi na ameanza kuzungumza na wataalamu kutoka kampuni ya Philips ya Uholanzi ili waweze kuanza kutengeneza mashine hizi, wameanza mazungumzo leo, kuanzia kesho tutaanza kuona mabadiliko yakifanyika, tutahakikisha suala hili linafanyiwa kazi kwa muda uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma” Eligaesha
Wagonjwa wanaotumia mashine za MRI kwa siku ni wagonjwa 10 hadi 15 na kila mgonjwa hutumia zaidi ya dakika 40 kutumiwa na kipimo cha CT Scan wagonjwa wenye uhitaji ni kati ya 20 hadi 25..“Wagonjwa wamekuwa wakipata taabu sana baada ya mashine hizi kuharibika na imewabidi kwenda hospitali binafsi ili kuweza kupata vipimo ambavyo huku ni gharama zaidi ya hapa” Eligaisha.
Amesema kwa sasa wanafanya juu chini kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.
Pia amesema Serikali ndiyo ilisaini mkataba wa kutengeneza mashine hizo na ndio sababu wameweza kulipa fedha kwa ajili ya matengenezo hayo.
Share this article :
Posted by Unknown at 12:34 AM
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook
Labels: HABARI

0 comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

TAZAMA FCN TV LIVE


Live streaming video by Ustream

World News

Blog Archive

  • ▼  2015 (6)
    • ▼  November (6)
      • MARTIN KADINDA GEREZANI KWA JACKY CLIFF CHINA..
      • DR. MAGUFULI ANAWEZA KUMTEUA WAZIRI MKUU KUTOKA UP...
      • RAIS MAGUFULI AWAGEUKIA MUHIMBILI
      • Siku moja baada ya Rais Magufuli kwenda Muhimbili ...
      • Magazeti ya Tanzania leo Novemba 11, 2015 yameamka...
      • Misri yazuia ndege za shirika la Uingereza
Powered by Blogger.

Labels

  • HABARI
  • MAGAZETI
  • VIDEO MPYA

About Me

Unknown
View my complete profile
 
Designed : Created by | Spacerz Creation | @spacerz2
Copyright © 2015. fcntv - HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA
Created by @spacerz2
Powered by @spacerz2