fcntv

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
  • HOME
  • RATIBA ZA VIPINDI
  • UDHAMINI
    • PIGA SIMU
    • EMAIL
    • SMS
  • MALIPO YA HUDUMA
  • MATANGAZO
  • MATAWI YETU
    • Dodoma
    • Igunga
    • Kahama
  • HABARI
  • MAGAZETI
  • VIDEO MPYA

skip to main | skip to sidebar
Home » HABARI » Misri yazuia ndege za shirika la Uingereza

Misri yazuia ndege za shirika la Uingereza



Image copyrightEPA
Image captionWatu wengi tayari wamefika uwanja wa ndege
Serikali ya Misri imesimamisha safari za shirika la ndege la Easyjet ambalo lilikuwa limepangiwa kuwasafirisha baadhi ya Waingereza waliokwama mji wa Sharm el-Sheikh leo.
Ndege za shirika la Easyjet pamoja na ndege za mashirika ya Monarch, Thomson na British Airways ndizo zilizokuwa zimepangiwa kuwasafirisha Waingereza waliokuwa Sharm el-Sheikh baada ya Uingereza kusitisha safari za ndege za kuingia na kutoka mji wa Sharm el-Sheikh Jumatano.
Hii ni baada ya kuibuka kwa uwezekano kwamba huenda ndege ya Urusi iliyoanguka baada ya kupaa kutoka mji huo Jumamosi iliyopita ikiwa na abiria 224 ililipuliwa.
Taarifa hizo zimeshutumiwa na Urusi na Misri.
Maafisa wa Easyjet wamesema maafisa wa Misri hawakubali ndege za Uingereza zitue katika uwanja huo wa ndege.
Ndege mbili za shirika hilo zilizokuwa zimepangiwa kuondoka kutoka viwanja vya ndege vya Gatwick na Luton nchini Uingereza bado zitaondoka kama zilivyopangiwa.
Lakini maafisa wa Easyjet wamesema ndege nyingine zinazopanga kuondoka kutoka Uingereza kwenza Sharm el-Sheikh kuwachukua abiria hazitaweza kuhudumu.
Share this article :
Posted by Unknown at 12:07 PM
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook
Labels: HABARI

0 comments:

Post a Comment

Newer Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

TAZAMA FCN TV LIVE


Live streaming video by Ustream

World News

Blog Archive

  • ▼  2015 (6)
    • ▼  November (6)
      • MARTIN KADINDA GEREZANI KWA JACKY CLIFF CHINA..
      • DR. MAGUFULI ANAWEZA KUMTEUA WAZIRI MKUU KUTOKA UP...
      • RAIS MAGUFULI AWAGEUKIA MUHIMBILI
      • Siku moja baada ya Rais Magufuli kwenda Muhimbili ...
      • Magazeti ya Tanzania leo Novemba 11, 2015 yameamka...
      • Misri yazuia ndege za shirika la Uingereza
Powered by Blogger.

Labels

  • HABARI
  • MAGAZETI
  • VIDEO MPYA

About Me

Unknown
View my complete profile
 
Designed : Created by | Spacerz Creation | @spacerz2
Copyright © 2015. fcntv - HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA
Created by @spacerz2
Powered by @spacerz2