
Swali linalogonga vichwa vya waandishi mbalimbali na wananchi ni nani atateuliwa kuwa waziri mkuu???

Nimempata kwenye exclusive ya Dk.Tulia Ackson ambaye ni wakili wa serikali ambaye pia aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali kwenye utawala wa Jakaya Kikwete, anayo majibu haya kuhusu uwezekano wa serikali ya Tanzania kuongozwa na Waziri Mkuu ambaye anatoka chama cha upinzani >>> ‘Sheria inamwezesha kufanya hivyo lakini Katiba imeweka Masharti kwamba Waziri Mkuu atoke wapi, hayo masharti yako matatu.
- Ni lazima Waziri Mkuu atoke katika Wabunge wa kuchaguliwa kutoka Majimboni.
- Ni lazima atoke chama chenye Wabunge wengi Bungeni, maana yake ni kwamba Rais akimteua Waziri Mkuu kutoka chama chenye Wabunge wengi ni lazima ataungwa mkono… lazima Waziri Mkuu aungwe mkono na Wabunge wengi.
- Ikitokea hakuna chama chenye Wabunge wengi Bungeni, Rais anaruhusiwa kuteua mtu yoyote ambaye ni Mbunge toka Bungeni.. awe ni Mbunge anayeungwa mkono na Wabunge wengi‘ >>> Dk.Tulia Ackson
0 comments:
Post a Comment