DR. MAGUFULI ANAWEZA KUMTEUA WAZIRI MKUU KUTOKA UPINZANI??????

Swali linalogonga vichwa vya waandishi mbalimbali na wananchi ni nani atateuliwa kuwa waziri mkuu???

Nimempata kwenye exclusive ya Dk.Tulia Ackson ambaye ni wakili wa serikali ambaye pia aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali kwenye utawala wa Jakaya Kikwete, anayo majibu haya kuhusu uwezekano wa serikali ya Tanzania kuongozwa na Waziri Mkuu ambaye anatoka chama cha upinzani >>> ‘Sheria inamwezesha kufanya hivyo lakini Katiba imeweka Masharti kwamba Waziri Mkuu atoke wapi, hayo masharti yako matatu.
- Ni lazima Waziri Mkuu atoke katika Wabunge wa kuchaguliwa kutoka Majimboni.
- Ni lazima atoke chama chenye Wabunge wengi Bungeni, maana yake ni kwamba Rais akimteua Waziri Mkuu kutoka chama chenye Wabunge wengi ni lazima ataungwa mkono… lazima Waziri Mkuu aungwe mkono na Wabunge wengi.
- Ikitokea hakuna chama chenye Wabunge wengi Bungeni, Rais anaruhusiwa kuteua mtu yoyote ambaye ni Mbunge toka Bungeni.. awe ni Mbunge anayeungwa mkono na Wabunge wengi‘ >>> Dk.Tulia Ackson
Labels:
HABARI
RAIS MAGUFULI AWAGEUKIA MUHIMBILI

Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili sambamba na kumsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Hussein Kidantu na kumteua Prof. Lawrence Mseru kushika nafasi hiyo.
Kati ya maagizo Rais aliyoacha ni pamoja na mashine za CT Scan pamoja na MRIkuhakikisha zinatengenezwa ndani ya wiki mbili.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaisha amesema baada ya kukutana na kamati tendaji ya hospitali hiyo leo na Kaimu Mkurugenzi aliyeteuliwa Prof.Lawrence Mseru ametoa maelezo na kuhakikisha watafanyia kazi maagizo
Yaliyotolewa na Rais ndani ya muda waliopewa.
“Tayari suala la CT Scan na MRI limeanza kufanyiwa kazi na ameanza kuzungumza na wataalamu kutoka kampuni ya Philips ya Uholanzi ili waweze kuanza kutengeneza mashine hizi, wameanza mazungumzo leo, kuanzia kesho tutaanza kuona mabadiliko yakifanyika, tutahakikisha suala hili linafanyiwa kazi kwa muda uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma” Eligaesha
Wagonjwa wanaotumia mashine za MRI kwa siku ni wagonjwa 10 hadi 15 na kila mgonjwa hutumia zaidi ya dakika 40 kutumiwa na kipimo cha CT Scan wagonjwa wenye uhitaji ni kati ya 20 hadi 25..“Wagonjwa wamekuwa wakipata taabu sana baada ya mashine hizi kuharibika na imewabidi kwenda hospitali binafsi ili kuweza kupata vipimo ambavyo huku ni gharama zaidi ya hapa” Eligaisha.
Amesema kwa sasa wanafanya juu chini kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.
Pia amesema Serikali ndiyo ilisaini mkataba wa kutengeneza mashine hizo na ndio sababu wameweza kulipa fedha kwa ajili ya matengenezo hayo.
Labels:
HABARI
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 11, 2015 yameamka na hizi kwenye Udaku, Michezo na hardnews

Story zote za magazeti leo alhamisi Novemba 11, 2015 ni hapa
Misri yazuia ndege za shirika la Uingereza

Serikali ya Misri imesimamisha safari za shirika la ndege la Easyjet ambalo lilikuwa limepangiwa kuwasafirisha baadhi ya Waingereza waliokwama mji wa Sharm el-Sheikh leo.
Ndege za shirika la Easyjet pamoja na ndege za mashirika ya Monarch, Thomson na British Airways ndizo zilizokuwa zimepangiwa kuwasafirisha Waingereza waliokuwa Sharm el-Sheikh baada ya Uingereza kusitisha safari za ndege za kuingia na kutoka mji wa Sharm el-Sheikh Jumatano.
Hii ni baada ya kuibuka kwa uwezekano kwamba huenda ndege ya Urusi iliyoanguka baada ya kupaa kutoka mji huo Jumamosi iliyopita ikiwa na abiria 224 ililipuliwa.
Maafisa wa Easyjet wamesema maafisa wa Misri hawakubali ndege za Uingereza zitue katika uwanja huo wa ndege.
Ndege mbili za shirika hilo zilizokuwa zimepangiwa kuondoka kutoka viwanja vya ndege vya Gatwick na Luton nchini Uingereza bado zitaondoka kama zilivyopangiwa.
Lakini maafisa wa Easyjet wamesema ndege nyingine zinazopanga kuondoka kutoka Uingereza kwenza Sharm el-Sheikh kuwachukua abiria hazitaweza kuhudumu.
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Posts (Atom)